Sunday, March 19, 2023

Friday, March 3, 2023

KATIBU WA NEC-ITIKADI NA UENEZI NDUGU SOPHIA MJEMA AMESEMA WANACCM HATUTANYAMAZA KWA HAYA MAKUBWA ANAYOFANYA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN


Na Mwandishi Wetu

NAKIVONA MEDIA


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Ndugu Sophia Mjema  amesisitiza kuwa wanaCCM kamwe wasikubali kunyamaza bali waendelee kusemea haya makubwa na mazuri yote yanayofanywa na Serikali  ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Mjema ameyasema hayo Jana Alhamisi Machi 02, 2023 kwenye mwendelezo wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo na Sekretarieti yake kwenye wilaya ya Mkalama mkoani Singida. 


"Tunae Mama (Rais Samia) anayetujali, anayetuletea maendeleo na hatuwezi kunyamaza. Nani atanyamaza kama Serikali yake inampa mtoto wake elimu bila kulipa, utanyamaza kama mkeo ameenda hospitali amepata sehemu nzuri ya kujifungua utanyamaza? utanyamaza wakati mbolea imeshushwa tulikuwa tunanunua Laki 1 na 50 hadi 60 leo kwasababu ya ruzuku aliyotoa Rais Samia kwenye mbolea tunanunua mbolea kwa Elfu 70." Alihoji Mjema.


Mwenezi Mjema ameendelea kusema CCM itaendelea kumuunga mkono Rais Samia na kumsemea kwasababu CCM ndiyo Chama kilichoshika Dola na kinachoongoza Serikali na kina jukumu la kusema haya.

Thursday, March 2, 2023

MWENEZI SOPHIA MJEMA AWATAKA WANA CCM WASIWE NA KIGUGUMIZI KUSEMEA SERA ZAKE KWA WATANZANIA WOTE.

 

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Sophia Mjema amesema wanaCCM wote nchini wanalo jukumu la kuelewa sera, itikadi za CCM na miradi ya Serikali inayotekelezwa na Serikali ya CCM na kuieneza kwa Watanzania wote bila kigugumizi chochote kile. Mjema ameyasema hayo leo Machi 01, 2023 kwenye mwendelezo wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo na Sekretarieti yake kwenye mkoa wa Singida akiwa kwenye tawi na 6 lililopo kijiji cha Ulemo kata ya Ulemo Wilayani Iramba kwenye mkutano wa tawi. "WanaCCM tusiwe na kigugumizi katika kusemea sera, itikadi ya CCM pamoja na miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ya CCM na kuieneza kwa wananchi ili waelewe kazi kubwa inayofanywa. Tusiposema sisi wanaCCM namna sera zetu zinavyotatua changamoto za huduma za kijamii na kuimarisha miundombinu basi watakuja wengine kusema kwa namna isiyo nzuri." Alisema Mjema. "WanaCCM tuelewe itikadi ya CCM ya ujamaa na kujitegemea na sera zetu nzuri zinazoshusha maendeleo makubwa na kueneza Chama chetu kwa wananchi. Kazi ya MwanaCCM ni kueneza na kutetea kazi kubwa hii inayofanywa kwenye nchi yetu na wanaCCM tutambe mbele za watu tukieleza haya bila kuwa na kigugumizi chochote kile." Alisisitiza Mwenezi Mjema amesisitiza kwamba CCM itaendelea kushusha elimu ya sera zake, itikadi yake pamoja na miradi mikubwa inayotekelezwa kwa Viongozi wake wapya waliochaguliwa hivi karibuni ili wawe na uelewa nazo ili waweze kuzieneza na kuzinadi kwa Watanzania nchi nzima sababu CCM ndiyo Chama tawala na hivyo ni lazima wananchi waelewe uelekeo wa Chama hiki.

Friday, February 24, 2023

Waziri WA Afya,Mhe.Ummy Mwalimu (Mb)


 

RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Mhe.SAMIA SULUHU



 

Wednesday, February 15, 2023

KATIBU MKUU NEC ITIKADI NA UENEZI NDUGU SOPHIA MJEMA


 

Sunday, February 5, 2023

MOROGORO


 Morogoro


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amehutubia mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Ndege Mkoani Morogoro katika kilele cha kuadhimisha sherehe za Miaka 46 ya Kuzaliwa kwa CCM Mkoani humo.
Sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa CCM aliambatana pia na Katibu Mkuu NEC, ITIKADI na Uenezi ndugu Sophia Mjema ambaye alizungumza na wanachama wa CCM wakiwemo wanachi wa vyama mbambali waliohudhuria kilele hicho.

#CCMImara
#KaziIendelee





Saturday, February 4, 2023

MKUTANO WA HADHARA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) FEBRUARI 05,2023



 

KATIBU WA NEC-ITIKADI NA UENEZI Ndg SOPHIA MJEMA






 

Friday, February 3, 2023

#KUMBUKIZI