Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Daniel Chongolo akiwa na KATIBU MKUU NEC, ITIFAKI NA UENEZI Ndugu SOPHIA MJEMA wakiendelea na ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM na Kusikiliza Kero Mbalimbali za wananchi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Morogoro, leo Januari 29, 2023, wamepokelewa wilayani Mvomero, akitokea Wilaya ya Gairo. 

Baada ya mapokezi katika eneo la Dumila, Ndg. Chongolo na Mjema  wameshiriki Mkutano wa Shina. Na. 18, Tawi la Dumila na kukagua ujenzi wa mradi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Zahanati ya Dumila.


Katika Ziara hiyo Katibu mkuu na MWENEZI wa CCM wameambatana pia na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Ndg. Issa Haji Gavu.


 
Top